
Kiswahili · PDF · 44 pages · Updated October 2026
TZS 2,000
Kitabu hiki ni kielelezo kikuu cha ukomavu na ukamilifu wa Sheria ya Kiislamu (Sharia) unadhihirisha uwezo wake wa kukusanya masuala mamilioni ya kisheria na kuyasawazisha chini ya misemo mifupi, mizito na yenye kubeba maana pana sana. Misemo hii ndiyo inayojulikana kama Kanuni za Fiqhi (Al-Qawa'id al-Fiqhiyyah).
Katika lugha ya kiakademia, Qawa'id (wingi wa neno Qa'idah) maana yake ni misingi au nguzo za jengo. Katika istilahi ya kisheria, ni hukumu ya kijumla inayotumika kwa masuala mengi madogo madogo (furu') ili kujua hukumu zake. Kitabu hiki kinalenga kuchambua kanuni hizi ambazo zinampa mwanasheria, kadhi, na mtafiti uwezo wa kuona picha kubwa ya Sharia bila kupotea katika maelezo mengi ya matawi.

Guidance Cordinator
Kama nyuki anayezunguka takribani maua 3000-4,000 ili kutengeneza mililita moja ya asali ambayo mnywaji anaweza kunywa mara moja na kuimaliza, vivyo hivyo waandishi huzunguka vyanzo vingi vya maarifa na tafsiri wakikusanya vipande vidogo vya hekima na kuviunganisha kwa juhudi kubwa, na msomaji hunufaika kwa kitabu kimoja ambacho anaweza kukisoma na kukimaliza mara moja; hivyo, mfano huu unatosha kuwa motisha kwa wenye akili, na unafupisha kwa uwazi faida ya kusoma na kunufaika kutoka kwenye vitabu. Khalifa Loishorwaki Simion alizaliwa Arusha, Tanzania, na kwa sasa anaishi jijini Dar es Salaam. Ni mhitimu wa shahada ya kwanza kutoka Chuo Kikuu cha Al-Azhar, Cairo, Misri (mwaka 2020) – moja ya vyuo vikongwe na vyenye heshima kubwa zaidi duniani katika masomo ya dini ya Kiislamu. Elimu hii imemjengea msingi imara wa kuchambua na kufundisha masuala ya kidini kwa umahiri na uaminifu.
Visit Sheikh Khalifa L. Simion's shop →