
Kiswahili · PDF · 121 pages · Updated October 2026
Free
MTUME WANGU (S.A.W.) ni kitabu cha kipekee kinachoeleza kwa undani uzuri wa sura, tabia, na maisha ya Mtume Muhammad ï·º kwa ushahidi wa hadithi sahihi na simulizi za Masahaba.
Kimeandikwa kwa Kiswahili fasaha sambamba na nukuu za Kiarabu, kikichora taswira ya mwonekano wake, mavazi yake, tabia zake tukufu, miujiza yake, na mapenzi ya kweli kwa kipenzi chetu.
Vipengele vya kuvutia ndani ya kitabu:
Maelezo ya kina ya mwonekano wa Mtume ï·º: uso, macho, nywele, tabasamu na haiba yake.
Tabia zake tukufu: ukweli, msamaha, huruma, na uaminifu.
Miujiza na matukio ya kipekee yaliyoshuhudiwa na Masahaba.
Dalili za Kiyama alizozitaja Mtume ï·º.
Njia za kuonyesha upendo na mapenzi ya kweli kwa Mtume wetu.
Kitabu hiki si simulizi tu, bali ni mwongozo wa kiroho unaoamsha mapenzi na heshima kwa Mtume ï·º, na ni hazina kwa kila Muislamu anayetaka kumfahamu na kumuiga katika maisha ya kila siku.

Guidance Cordinator
Kama nyuki anayezunguka takribani maua 3000-4,000 ili kutengeneza mililita moja ya asali ambayo mnywaji anaweza kunywa mara moja na kuimaliza, vivyo hivyo waandishi huzunguka vyanzo vingi vya maarifa na tafsiri wakikusanya vipande vidogo vya hekima na kuviunganisha kwa juhudi kubwa, na msomaji hunufaika kwa kitabu kimoja ambacho anaweza kukisoma na kukimaliza mara moja; hivyo, mfano huu unatosha kuwa motisha kwa wenye akili, na unafupisha kwa uwazi faida ya kusoma na kunufaika kutoka kwenye vitabu. Khalifa Loishorwaki Simion alizaliwa Arusha, Tanzania, na kwa sasa anaishi jijini Dar es Salaam. Ni mhitimu wa shahada ya kwanza kutoka Chuo Kikuu cha Al-Azhar, Cairo, Misri (mwaka 2020) – moja ya vyuo vikongwe na vyenye heshima kubwa zaidi duniani katika masomo ya dini ya Kiislamu. Elimu hii imemjengea msingi imara wa kuchambua na kufundisha masuala ya kidini kwa umahiri na uaminifu.
Visit Sheikh Khalifa L. Simion's shop →