
Udhu, Kuoga na Tayamum
Kiswahili · PDF · 12 pages · Updated October 2026
Free
Kitabu Namna ya Swala kwa Picha ni mwongozo wa kipekee unaoeleza hatua kwa hatua namna ya kuoga (ghusl), kutawadha, kufanya tayammum na kuswali kwa usahihi kulingana na mafundisho ya Mtume ï·º. Kimeandikwa kwa Kiswahili fasaha na kimepambwa kwa michoro rahisi inayomsaidia msomaji kufuatilia kila hatua kwa macho na vitendo.
Vipengele vya kuvutia ndani ya kitabu:
Maelezo ya wazi na mafupi, yanayoweza kufuatwa na kila Muislamu.
Michoro na vielelezo vinavyorahisisha uelewa wa vitendo vya ibada.
Dua na dhikri muhimu baada ya swala.
Muhtasari wa sunna zilizopangiliwa (Rawaatib) kwa maisha ya kila siku.
Kitabu hiki ni msaada bora kwa wanafunzi, walimu, na kila Muislamu anayetaka kujifunza au kukumbushwa namna ya kuswali kwa usahihi. Ni nyenzo ya thamani kwa madrasa, familia na wasomaji binafsi.
6 chapters

Guidance Cordinator
Kama nyuki anayezunguka takribani maua 3000-4,000 ili kutengeneza mililita moja ya asali ambayo mnywaji anaweza kunywa mara moja na kuimaliza, vivyo hivyo waandishi huzunguka vyanzo vingi vya maarifa na tafsiri wakikusanya vipande vidogo vya hekima na kuviunganisha kwa juhudi kubwa, na msomaji hunufaika kwa kitabu kimoja ambacho anaweza kukisoma na kukimaliza mara moja; hivyo, mfano huu unatosha kuwa motisha kwa wenye akili, na unafupisha kwa uwazi faida ya kusoma na kunufaika kutoka kwenye vitabu. Khalifa Loishorwaki Simion alizaliwa Arusha, Tanzania, na kwa sasa anaishi jijini Dar es Salaam. Ni mhitimu wa shahada ya kwanza kutoka Chuo Kikuu cha Al-Azhar, Cairo, Misri (mwaka 2020) – moja ya vyuo vikongwe na vyenye heshima kubwa zaidi duniani katika masomo ya dini ya Kiislamu. Elimu hii imemjengea msingi imara wa kuchambua na kufundisha masuala ya kidini kwa umahiri na uaminifu.
Visit Sheikh Khalifa L. Simion's shop →