
Kiswahili ยท PDF ยท 41 pages ยท Updated September 2026
TZS 2,300
Zaka si tu wajibu wa kidini bali ni njia ya kusafisha mali, kuimarisha undugu wa Kiislamu, na kupunguza pengo kati ya matajiri na maskini. Hata hivyo, wengi wa Waislamu leo wanakumbana na maswali magumu: Je, nisabu ni kiasi gani? Zaka ya mshahara inatolewaje? Je, akiba za M-Pesa, hisa, au Bitcoin zinatozwa zaka?
Kitabu hiki kimeandaliwa kwa lugha rahisi na mifano ya kihesabu ya vitendo, kikimwongoza msomaji hatua kwa hatua kuanzia misingi ya zaka hadi masuala magumu ya kisasa. Miongoni mwa yale utakayojifunza:
Maana, dalili, na umuhimu wa zaka โ pamoja na tofauti yake na sadaka
Masharti saba ya kutolewa zaka
Aina za mali zinazotozwa zaka: dhahabu na fedha, biashara, mazao ya kilimo, na mifugo
Jinsi ya kukokotoa nisabu na kiwango cha malipo, kwa mifano ya shilingi za Tanzania
Masuala ya kisasa: mshahara, akiba za benki na mitandao, biashara za mtandaoni, hisa, pensheni, na cryptocurrencies
Wanaostahiki kupokea zaka (asnaf) na faida zake za kiroho, kijamii, na kiuchumi
Kitabu hiki ni rafiki kwa kila Muislamu anayetaka kutekeleza ibada hii kwa uelewa na uhakika โ mwanafunzi, mfanyabiashara, au mtu yeyote mwenye shauku ya kujifunza dini yake vizuri zaidi.
Toleo la Kwanza โ Februari 2026

Guidance Cordinator
Kama nyuki anayezunguka takribani maua 3000-4,000 ili kutengeneza mililita moja ya asali ambayo mnywaji anaweza kunywa mara moja na kuimaliza, vivyo hivyo waandishi huzunguka vyanzo vingi vya maarifa na tafsiri wakikusanya vipande vidogo vya hekima na kuviunganisha kwa juhudi kubwa, na msomaji hunufaika kwa kitabu kimoja ambacho anaweza kukisoma na kukimaliza mara moja; hivyo, mfano huu unatosha kuwa motisha kwa wenye akili, na unafupisha kwa uwazi faida ya kusoma na kunufaika kutoka kwenye vitabu. Khalifa Loishorwaki Simion alizaliwa Arusha, Tanzania, na kwa sasa anaishi jijini Dar es Salaam. Ni mhitimu wa shahada ya kwanza kutoka Chuo Kikuu cha Al-Azhar, Cairo, Misri (mwaka 2020) โ moja ya vyuo vikongwe na vyenye heshima kubwa zaidi duniani katika masomo ya dini ya Kiislamu. Elimu hii imemjengea msingi imara wa kuchambua na kufundisha masuala ya kidini kwa umahiri na uaminifu.
Visit Sheikh Khalifa L. Simion's shop โ